Bei moja kwa kila kifurushi.
Hakuna mshangao.
Ukiuza rejareja, jumla au vyote viwili, bei ni ile ile. Anza bure, na ulipe pale tu Duka365 inapoendesha duka lako kweli.
Kwa kuanza
Bure kwa muda wowote unaotaka
- Hadi bidhaa 100
- Mauzo 150 kwa mwezi
- Rejareja, jumla au vyote viwili
- Ufuatiliaji wa bidhaa na tarehe za mwisho
- Mtumiaji mmoja — mmiliki wa duka
Arifa za SMS hazijumuishwi
Kwa duka linalouza kila siku
- Bidhaa na mauzo bila kikomo
- Ripoti za kina na ufuatiliaji wa faida
- Hadi wanatimu 5
- Kuingiza CSV na kuhamisha data
- Picha za bidhaa
- Matumizi ya API
- Simamia biashara kadhaa kwa akaunti moja
Inajumuisha arifa 200 za SMS kwa mwezi
Bei hazijumuishi VAT.
Kwa timu na matawi mengi
- Kila kitu cha Pro
- Matawi bila kikomo
- Ugawaji na uhamishaji wa bidhaa kati ya matawi
- Wafanyakazi, bidhaa na ripoti kwa kila tawi
- Sell Out Intelligence — uchambuzi wa mahitaji na kuagiza upya
- Wanatimu bila kikomo
- Msaada wa kipaumbele
- Ghala 1 na gari 1, pamoja na zamu za magari na ulinganishaji wa hesabu
Inajumuisha arifa 1,000 za SMS kwa mwezi
Bei hazijumuishi VAT.
Kwa wasambazaji wanaosimamia maghala, magari na timu za mauzo ya nje.
Maghala, magari na mauzo ya nje — yote sehemu moja.
- Maghala mengi
- Stoo ya magari na mauzo ya nje
- Uza bila intaneti, taarifa zisawazishwe baadaye
- Mauzo ya mkopo na makusanyo ya madeni
- Ulinganishaji wa hesabu za bidhaa na fedha
- Ruhusa na majukumu kwa wafanyakazi wa ghala, wauzaji na wahasibu
- Msaada wa kuanza kutumia mfumo na huduma ya kipaumbele
Bei inapangwa kulingana na idadi ya maghala na magari yanayotumika. Hakuna malipo kwa kila mtumiaji. Bei hazijumuishi VAT.
Kila duka jipya linaweza kujaribu kifurushi cha Business bure kwa siku 14 wakati wowote likiwa tayari — unaanzisha mwenyewe ndani ya programu, hivyo muda unaanza pale wewe unapoanza. Bei hazijumuishi VAT.
Kutoka ghalani, garini hadi kwa mteja.
Kila shilingi inahesabiwa.
Kwa wasambazaji. Simamia maghala, stoo ya magari, mauzo ya nje, madeni na ulinganishaji wa hesabu kwenye mfumo mmoja — badala ya kutumia majedwali ya Excel, madaftari ya stoo na karatasi za kulinganisha hesabu.
Gharama ya kuanzisha mfumo na kukusaidia kuanza kuutumia inategemea ukubwa na mahitaji ya biashara yako. Tunakusaidia kuhamisha bidhaa, stoo, maghala na timu yako kwenda Duka365 hadi mfumo uwe tayari kutumika.
Programu yenye chapa yako (hiari) — jina, nembo na rangi za kampuni yako kwenye programu inayotumiwa na timu yako. Tuulize kuhusu huduma hii. Zungumza nasi
Enterprise — Unahitaji programu yenye jina na nembo ya kampuni yako, kuunganisha mifumo mingine au makubaliano maalumu ya huduma (SLA)?
Kila kifurushi kina nini
Kila kifurushi kinaendesha duka zima. Vifurushi vinavyolipiwa vinaondoa mipaka na kuongeza vitu vinavyokuwa na maana pale unapokuwa na wafanyakazi, matawi kadhaa, au msambazaji anayeomba takwimu.
| Bure | Pro | Business | DISTRIBUTION | |
|---|---|---|---|---|
| Bidhaa kwenye orodha yako | 100 | Bila kikomo | Bila kikomo | Bila kikomo |
| Mauzo kwa mwezi | 150 kwa mwezi | Bila kikomo | Bila kikomo | Bila kikomo |
| Watu wanaoweza kuingia | 1 | 5 | Bila kikomo | Bila kikomo |
| Meseji za tahadhari | — | 200 kwa mwezi | 1,000 kwa mwezi | 3,000 kwa mwezi |
| Matawi | 1 | 5 | Bila kikomo | Bila kikomo |
| Maghala | — | — | 1 | 10 |
| Magari | — | — | 1 | 15 |
| Kaunta, risiti na mapato ya siku | ||||
| Programu ya simu inayofanya kazi bila intaneti | ||||
| Hesabu za stoo na tahadhari za bidhaa zilizopungua | ||||
| Tarehe za mwisho wa matumizi na tahadhari za mapema | ||||
| Bei za jumla na rejareja, punguzo la idadi kubwa | ||||
| Wateja, mikopo na ufuatiliaji wa madeni | ||||
| Manunuzi na wasambazaji | ||||
| Kusoma barcode, kutengeneza barcode na lebo | ||||
| Vitabu: leja, mizania na faida na hasara | ||||
| Akaunti za wafanyakazi zenye majukumu tofauti | ||||
| Ripoti kamili, ikiwemo faida kwa kila bidhaa | ||||
| Malengo ya mapato na faida ya kila mwezi | ||||
| Kuhamisha taarifa zote kwenda Excel | ||||
| Kuingiza bidhaa nyingi kutoka lahajedwali | ||||
| API kwa ajili ya mifumo yako mwenyewe | ||||
| Sell Out Intelligence — nini uagize, nini kimekaa | ||||
| Kuhamisha stoo kati ya sehemu zako | ||||
| Zamu za magari na ulinganishaji wa hesabu za bidhaa na fedha |
DISTRIBUTION: kila ghala zaidi ya yaliyojumuishwa ni TSh 50,000 kwa mwezi, na kila gari linalotumika zaidi ya yaliyojumuishwa ni TSh 20,000 kwa mwezi.
Bei hazijumuishi VAT.
Jinsi bei inavyofanya kazi
Rejareja au jumla ni bei ile ile
Jinsi unavyouza inabadilisha skrini unazoona, si bili yako. Unaweza kubadilisha kati ya rejareja, jumla na vyote viwili wakati wowote, kwenye kifurushi chochote, bila kupoteza bidhaa, bei, wateja au historia ya mauzo.
Bei moja kwa duka zima
Unalipa kwa kila biashara, si kwa kila mtumiaji. Pro inajumuisha hadi wanatimu watano; Business haina kikomo. Duka la pili lina kifurushi chake tofauti.
Kwa nini SMS ina kikomo
Arifa za bidhaa kuisha, tarehe za mwisho na muhtasari wa kila siku ni ujumbe halisi tunaolipia mtandao. Kila kifurushi kina kiasi cha mwezi ili wanaotuma sana wasifadhiliwe kimyakimya na wengine. Kufikia kikomo hakukuzuii kuuza — kunasitisha arifa tu hadi tarehe 1.
Hakuna kadi, hakuna kukatwa kiotomatiki
Unalipa kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au benki kisha unarekodi namna ya muamala ndani ya programu. Hakuna kinachotolewa kwenye akaunti yako kiotomatiki, na hakuna kinachojirudia bila wewe kutuma.
Nini kinatokea usipolipa
Tunapendelea kukuambia sasa kuliko ugundue kwa kitufe kilichoacha kufanya kazi. Kifurushi kinapoisha, huduma zinapungua hatua kwa hatua kwa mwezi mmoja, na unajulishwa kila hatua.
- 01
Siku 3 za kwanza
Hakuna kinachobadilika. Unaona ukumbusho ndani ya programu, na kila kitu kinaendelea kama kawaida.
- 02
Baada ya siku 3
Arifa za SMS na matumizi ya API yanasitishwa — hivyo ndivyo vitu viwili vinavyotugharimu pesa kila vinapotumika. Ripoti, kuhamisha data, timu yako na huduma nyingine zote zinaendelea.
- 03
Baada ya siku 7
Duka lako linahamia vikomo vya kifurushi cha bure na huduma za malipo zinasitishwa. Unabaki na kila bidhaa, mauzo, mteja na ripoti uliyonayo — huwezi tu kuongeza zaidi ya vikomo vya bure hadi ulipe.
- 04
Baada ya siku 30
Duka linaacha kupokea maingizo mapya — hakuna bidhaa, wasambazaji, wateja au matumizi mapya. Bado unaweza kurekodi mauzo, kusoma kila kitu na kuhamisha data. Hakuna kinachofutwa, na ukilipa kila kitu kinafunguka mara moja.
Mambo matatu hatutafanya
- Hatutakuzuia kurekodi mauzo. Si siku ya 8, si siku ya 60 — mashine inayomkatalia mteja aliyesimama mbele yako si kitu ambacho malipo yaliyochelewa yanapaswa kusababisha.
- Hatutafuta data yako kwa sababu ya bili ambayo haijalipwa.
- Hatutazuia kuhamisha data yako. Vitabu vyako ni vyako, na unaweza kuvitoa wakati wowote, hata wakati akaunti yako ina deni.
Maswali ya kawaida
- Naweza kubadilisha kifurushi baadaye?
- Ndiyo, wakati wowote. Ukipanda katikati ya mwezi unalipa tofauti kwa siku zilizobaki tu. Ukishuka, thamani ya siku ambazo hujazitumia inawekwa kwenye akaunti yako kama salio la malipo yanayofuata.
- Naweza kurudishiwa pesa zangu?
- Hapana. Malipo hayarudishwi, uwe umelipia mwezi au mwaka. Unaweza kusitisha wakati wowote kabla ya malipo yanayofuata: unaendelea kutumia ulicholipia hadi muda huo uishe, na hakuna malipo zaidi.
- Nini kinatokea nikifika kikomo cha kifurushi cha bure?
- Kwenye kifurushi cha bure kikomo cha mauzo ni kizuizi halisi — utahitaji kuhamia Pro ili kuendelea kurekodi mauzo mwezi huo. Kila ulichoingiza kinabaki pale pale.
- Nalipaje hasa?
- Tuma kiasi kwa M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au benki, kisha rekodi namba ya muamala chini ya Kifurushi na Malipo. Tunaihakiki kwenye taarifa yetu na kuithibitisha, mara nyingi siku hiyo hiyo.
- Nina maduka mawili. Nalipa mara mbili?
- Kila biashara ina kifurushi chake, kwa sababu kila moja ina bidhaa, wafanyakazi na ripoti zake. Pro na Business zinakuwezesha kusimamia biashara kadhaa kwa kuingia mara moja tu.
- Nasitishaje?
- Tuambie, au usilipie kipindi kinachofuata. Fanya hivyo kabla ya malipo yanayofuata. Hakuna kinachojirudia chenyewe kwa sababu hakuna kadi iliyohifadhiwa. Kifurushi chako kinaendelea hadi mwisho wa muda uliolipia, kisha duka lako linapungua kwa hatua zilizoelezwa hapo juu na data yako inabaki tayari kuhamishwa.
Anza bure leo
Hakuna kadi, hakuna ahadi. Ongeza bidhaa zako na uone kama inafaa duka lako kabla ya kulipa chochote.